Virusi vya Computer

ZIJUE AINA ZA VIRUS VYA KOMPYUTA

 AINA ZA VIRUS VYA KOMPYUTA


kuna aina tofauti tofauti za virus vya kompyuta ambavyo vinaweza kugawanyika kulingana na asili yao ,aina ya mafaili wanayoathiri ,namana wanavyoshambulia kompyuta au namna ambavyo wanasababisha madhara katika programu kuu yaani Operating system .Embu tuangalie kwa undani aina hizi za virusi

Resident Viruses
aina hii ya virusi hukaa moja kwa moja katika aina ya memory aina ya RAM .Kutoka hapa basi huweza kuathiri  mfumo mzima wa kompyuta ,huaribu mafail pale yanapofunguliwa au kufungwa au kurudufiwa au hata kubadilishwa jina

Mifano ya aina hii ya virus ni kama : Randex, CMJ, Meve, and MrKlunky.

Direct Action Viruses
lengo kuu la virusi vya aina hii ni kuharibu au kuathiri pale tu vinapofunguliwa ,plae mabapo hali fulani zinapotengenezwa .Hawa hushambulia mafolda na kuyafnaya yasiweze kufunguka
Overwrite Viruses

aina hii ya virusi huwa na sifa ya kufuta taarifa zinazokuwa katika mafail husika  na kuyafanya yasiwe na maana tena .NJia pekee ya kuwaondo aina hii ya virus ni kwa kuliondoa faili husika lote yaani ku delete
mfano wa aina hii ya virusi ni : Way, Trj.Reboot, Trivial.88.D.
Boot Virus
aina hii ya virusi huathiri sehemu za vitunza taarif mfano Hard disk au floppy disk ambazo huitwa kwa kitaalamu Boot sector.Hii ni sehemu muhimu sana ya diski kufanya kazi  na ndio inayofanya program iweze kufanya kazi yaani booting .Njia pekee ya kuzuia aina hii ya virusi ni kuhakikisha unalinda diski zao yaani Right protect au usianzishe(kuwasha ) kompyuta wakati ikiwa na floppy diski ndani yake
mfano wa aina hii ya virus: Polyboot.B, AntiEXE.
Macro Virus
hawa ni aina ya virus wanatengenezwa kwa kutumia aina fulani za programu ambazo zinabeba vitu vinavyoitwa macros .Hivi huleta madhara makubwa katika kompyuta husika .Hizi programu hufanya program nyingi ziwe zinajiendesha zenyewe kama programu moja kwa pamoja na hivyo huifanya kompyuta yako kuw nzito
mfano wa aina hii ya virus ni  Relax, Melissa.A, Bablas, O97M/Y2K.

Directory Virus
hawa hubadilisha njia ya faili husika kuna wakati utapata message "File not found" au "directory path not found" kwa kulifungua file lolote ambalo litakuwa limeliwa na kirusi basi utakuwa umehamsha aina hii ya kirusi huwa mara nyingi mafaili hayo yaliyoliwa hutambulika kwa  ekstensheni .EXE  au .COM

File Infectors
aina hii ya virusi kama ilivyo kwa huathiri mafaili yenye file ekstensheni ya .EXE ao >COM  hivyo hufanya kama ni program ishindwe kufunguka

Worms
worm ni aina ya programu na hufanana na virusi isipokuwa worms zinatabia ya kujiongeza zenyewe idadi na huleta matokeo hasi katika kompyuta ,kizuri ni kwamba zinatambulika kirahisi (detected ) na kusafishwa na antivirus nyingi tu
mifano ya minyoo hii ya kompyuta ni : PSWBugbear.B, Lovgate.F, Trile.C, Sobig.D, Mapson.
hawa antivirus wana njia nyingi za kuingia hivyo chukua tahadhari katika matumizi yako ya kompyuta kwana kwa kuhakikisha unakuwa na kilinda virus yaani antivirus .
zipo antivirus za aina nyingi sana lakini zio zote zinaweza kuondoa virus
TAHADHARI: Zipo antivirus nyingine hasa hizi zitolewazo bure huwa ni virus ni si antivirus omba ushauri kwa wataalamu kupata antivirus nzuri na itakayo kufaa kulingana na aina aya kompyuta uliyonayo
hizi ni aina kadhaa za antivirus ambazo zimethibitishwa kuwa ni nzuri kwa matumizi ya kompyuta nyingi

No comments:

Post a Comment